Mihogo ya kukaanga na chachandu


Karibuni tena jikoni kwetu tuandae vitafunio leo, mihogo ya kukaanga, natumai sikitu kigeni kwetu. Sio siri wakati mwengine tubadili vitafunio, mambo ya kila siku mikate na maandazi vinachosha walaji. Siku nyengine chemsha viazi, siku nyengine ndizi, siku nyengine kaanga mihogo kama hivi na andaa kachumbari yake kuleta hamu ya kuila.

Ingredients

  • Mihogo mikubwa 3
  • mafuta lita 1
  • kitunguu 1
  • thoum kiasi
  • tangawizi kiasi
  • nyanya 4
  • limao 1
  • karoti nusu
  • hoho nusu
  • pilipili manga kidogo
  • chumvi
  • pilipili mbichi

Directions

  1. Menya mihogo, ikatekate kiasi upendacho na kwa urahisi wa kuiva kisha ikoshe
  2. bandika karai, tia mafuta, yakipata moto weka mihogo ukaange, angalia moto usiwe mkali sana ili mihogo iive polepooe bila kubabuka
  3. ikishaiva itoe uitie kwenye chujio ijichuje mafuta. Anza kuandaa kachumbari yakulia mihogo.
  4. osha nyanya, karoti, hoho, tangawizi, chukua sufuria uvisage uvitie, kisha katakata kitunguu tia, twanga pilipili uitie pia. Weka chumvi na pilipili manga.
  5. bandika jikoni ueke na maji nusu kikombe na unyunyuzie mafuta kiasi. Funika acha ichemke kiasi dakika 5
  6. Kisha tia limau uache ichemke kidogo, epua kachumbari yetu yakulia mihogo tayari.
Sasa mihogo yetu twaweza kuila muda wowote, kwa chai, maji na hata juisi na hata ukipata samaki wakukaanga  hunoga mno. Nasio lazima uwe na kachumbari waweza kula na tomato, chilli sio mbaya, Karibuni sana.