Jinsi ya kupika Chapati za maji: Leo ninakuletea hatua kwa
hatua namna ya kuandaa na kupika Chapati laini. Tafadhali fuatana nami
katika pishi hili.
Pishi: Chapati za maji/laini
Utangulizi: chapati laini ni
kitafunwa au chakula kinachopendwa na na wengi. chakula hiki hupendwa
zaidi na watu kwa sababu ni rahisi kutayarisha..
Mahitaji
- Ngano 1/2 kilo
- mayai 3
- mafuta au samli 1/4 kikombe
- kitunguu kikubwa kilichosagwa 1
- Kitunguu Swaumu punje 4
- Chumvi 1/2kijiko au kulingana na matakwa yako
Mahitaji
Namna ya kupika chapati za maji
- Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi.
- Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito san a wala si mwepesi sana.
- Ongeza mayai na chunmvi endelea kukoroga.
- Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto.
- Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili.
- Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka iwe rangi ya kahawia.
- Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa.
- Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia
Kiasi hichi kinatosha kupika chapati laini sita Mpaka kumi. Chapati
za maji hupendeza zaidi kuliwa Michuzi mizito, Chai na kadhalika.