Jinsi ya kupika wali mseto



 Jinsi ya kupika wali mseto: Mseto ni mchanganyiko mzuri wa mchele na maharagwe. Ni chakula kitamu sana, rahisi kutayarisha na yenye gharama kidogo unayoweza kuimudu popote pale ulipo iwe mjini au kijijini. Kama umechoshwa na pilau, jaribu mlo huu kisha toa maoni yako hapo chini. Karibu tupike

Jinsi ya kupika wali Mseto hatua kwa hatua

Mahitaji

Kikombe kimoja cha maharagwe
  1. Mchele Vikombe viwili
  2. Vitunguu viwili vikubwa
  3. Kitunguu saumu/thomu kimoja
  4. Viungo mchanganyiko Nusu kijiko cha chai
  5. Nyanya moja yenye ukubwa wa kati
  6. Chumvi kiasi
  7. Karoti mbili
  8. Nazi moja

Jinsi ya Kuandaa

  1. Chagua vizuri na upike maharagwe lakini angalia yasiive sana yakawa rojo.
  2. Chagua vizuri na osha mchele wako.
  3. Menya vitunguu,osha na katakata
  4. Menya vitunguu saumu na twanga vilainike
  5. Osha karoti na katakata
  6. Kaanga vitunguu mpaka viwe na rangi ya kahawia
  7. Weka viungo mchanganyiko na nyanya na acha viive.
  8. Weka maji vikombe viwili na nusu au tui la nazi na chumvi kiasi.
  9. Acha ichemke,weka mchele na koroga kidogo.
  10. Ikikauka maji,ongeza maharagwe na changanya vizuri
  11. Punguza moto ili ikauke vizuri
  12. Weka moto juu na chini kidogo kwa dakika 15-30
  13. Chakula chako tayari kwa kupakuliwa
Dondoo:
Chakula hiki kinaweza kuliwa pamoja na saladi, vilevile waweza kushushia na kinyaji chochote kisichokuwa na gesi. Hivyo ndivyo jinsi ya kupika wali wa mseto. Asante kwa kutembelea.

1 comments:

Lazima nijaribu mapishi haya nimpikie mume wangu...(♥ω♥*)