Jinsi ya kupika ugali wa mahindi: Ugali ni chakula kinacholiwa sana Afrika ya Mashariki. Tokea nikiwa mdogo nimekuwa nikitumia chakula hiki hasa nyakati za mchana.
Leo nimekutayarishia ugali maarufu, Ugali wa unga wa mahindi. Nimejaribu kutafuta namna nyepesi ya kupika chakula hiki. fuatiliana nasi.
Mapishi ya: Ugali wa mahindi
Maandalizi na Mahitaji
Mahitaji
- Unga wa mahindi robo kilo (Gramu 240)
- Maji Nusu lita
Namna ya kupika hatua kwa hatua
Namna ya kupika Ugali
- Weka maji kwenye moto ili yachemke
- Tengeneza mchanganyiko kwa kutumia kiasi kidogo cha unga na maji kwenye bakuli pembeni
- Ongeza mchanganyiko wako huo kwenye maji yanayochemka
- Koroga vizuri kwa kutumia mwiko mpaka iwe uji ulioiva
- Ongeza unga uliobaki na uchanganye vizuri hadi iwe ngumu.
- Endelea kukoroga (kusonga), ukihakikisha hakuna mabonge hadi ugali uive vizuri.
- Epua na upakue ikiwa moto.
Dondoo
Maziwa freshi yanaweza kutumiwa badala ya maji
pamoja na siagi kidogo. Usiposonga (koroga) vizuri ugali utabaki na
mabonge bonge yenye unga ndani Maji yasipochemka vizuri kuna uwezekano
wa kutoka ugali mbichi. Ugali unaweza kuliwa na mbogamboga, Nyama za
kukaanga pamoja na achali na saladi, Ugali haupendezi kuliwa na mboga
zenye michuzi mingi.
Hivyo ndivyo jinsi ya kupika ugali wa unga wa mahindi. Asante kwa kutembelea blogu yetu.
Ugali huu unaweza kuliwa na watu : 2-3