Jinsi ya kupika visheti

Jinsi ya kupika visheti


Wadau wa jiko letu, leo tuna visheti, visheti ni aina ya kitafunwa, chaweza liwa na kahawa, chai, juisi na hata maji ukihaaliwa. Ila kwa chai na kahawa vinapendeza zaidi. Kuna nmna tofauti tofauti za uandaaji wa visheti, kukandia nazi, mara nyengine mafuta, waweza pia kukandia siagi na hata maziwa. Vya leo tutatumia siagi, na tukijaaliwa siku nyengine tutapika na hizo aina nyengine.

Ingredients

  • Ngano kilo1
  • mafuta lita1
  • siagi robo kilo
  • yai 1
  • Hiliki kiasi
  • baking powder kijiko1
  • Chumvi kidogo sana
  • Sukari nusu

Directions

  1. Chunga unga wako, weka baking powder, tia chumvi kidogo ukipenda, tia sukari kidogo na hiliki changanya na siagi uvuruge
  2. tia mafuta nusu kikombe, endelea kuvuruga unga wako
  3. piga yai litie kwenye unga, endelea kuvuruga
  4. ongeza maji kiasi ili unga wetu uweze kukandika na kushikana kuwa donge moja
  5. Tengeneza vidonge vidonge, kisha uviviringishe hadi viwe kama fimbo, baadae weka kwenye kibao ukatekate visheti vidogodogo
  6. Weka mafuta kwenye karai jikoni, yakipata moto kaanga visheti hadi viive, kisha vitoe pembeni uanze kuandaa SHIRA
  7. andaa shira kwa kutumia sukari nusu, na maji kikombe cha chupa ya chai kimoja, bandika jikoni maji ulotia sukari yachemke hadi yatoe povu na ukiitoa kidogo ukiishika inanata sana, hapo shira ni tayari
  8. mimina visheti ulokaanga kwenye sufuria ya shira, weka na hiliki, kisha vipetepete ili vijigeuze na kuenea sukari vyote. Vikiwa tayari vimekaukia sukari vizuri, visheti vyetu weka kwenye chombo tayari kumfikia mlaji
Visheti vyetu tayari wadau, mi huvipenda hivi vya kukandia siagi sababu hukaa muda mrefu bila kuwa vigumu. Kwa hiyo waweza tengeneza ukala na vikibaki unavihifadhi vizuri kwa ajili ya kutafuna sikunyengine.