Jinsi ya Kupika Vitumbua vya Nyama


  • Leo tena vitumbua, lakini hatutamia unga wa mchele kama tulivyozoea, bali nyama ya kusaga. Ni pishi zuri sana, ukiwa na juisi pembeni, vinapendeza sana kula muda wa jioni, ila waweza kula muda wowote wa nafasi yako. Haya jiweke tayari tuanze kuandaa pishi hili Tamu.

Pishi: Vitumbua vya Nyama

Mahitaji

  • Nyama ya kusaga robo
  • Kitunguu 1
  • Kitunguu thoum nusu kijiko
  • Karoti 1
  • Pilipili hoho nusu
  • Mayai 5-6
  • Baking powder nusu kijiko kidogo
  • Pilipili manga kiasi
  • Pilipili mbichi(ukipenda)
  • Chumvi kiasi

Namna ya kupika vitumbua vya nyama Hatua kwa hatua

  1. Safisha nyama, uitie thoum, chumvi, pilipili manga na tangawizi, ibandike jikoni ili iive na ikauke vizuri
  2. kata vitunguu, hoho, pilipili na uvichanganye na mayai, kisha vyote vitie kwenye nyama yetu
  3. Weka kwenye blender mchanyanyiko wetu uusage kidogo ila usiwe laini sana. Ikiwa tayari, mimina katika bakuli.
  4. Kisha tia baking powder, karoti na chumvi kidogo kisha changanya vizuri.
  5. andaa chuma cha kukaangia vitumbua, bandika jikoni, weka mafuta kidogo.
  6. Mafuta yakipata joto chota kwa upawa mchanganyiko wetu utie kwenye kikaango, vikiiva upande mmoja geuza na upande wa pili uive kisha uvitoe.
  7. Endelea kuchoma hadi viishe vyote, hapo tunakua tumemaliza upishi wetu wa vitumbua
Natumai tumeenda sambamba hatua kwa hatua jinsi ya kupika vitumbua vya nyama. Karibuni kwa maoni, maswali na ushauri hapo chini.