habari, leo jikoni tuna dagaa, chanzo kikubwa cha protini, ni kitoweo kizuri kwa afya zetu. Dagaa wabichi waweza wachemsha kupata supu, kuwakausha na hata kukaanga. Sisi leo tunakuja na jinsi ya kukaanga dagaa tayari kwa kula pamoja na ugali wetu pembeni Karibu.
Pishi: Dagaaa wa Kukaanga
Mahitaji
- dagaa wabichi vikombe 2
- mafuta ya kupikia nusu lita
- vitunguu thoum kijiko cha chai 1
- tangawizi kiasi
- pilipili mbichi 1
- pilipili manga 1
- chumvi kiasi
- ndimu au limao kubwa 1
Jinsi ya kuandaa na kupika
- Anza kwa kuwasafisha dagaa wako, na kuwatoa vichwa , wakishasafishika waeke kwenye chujio wachururike maji
- Saga thoum, tangawizi, pilipili manga na pilipili mbichi kisha uzitie kwenye dagaa pamoja na chumvi na limao uchanganye vizuri, wacha kwa kiasi robo saa dagaa wakolee viungo
- Bandika chuma cha kukaangia jikoni, tia mafuta, yakichemka watie dagaa ukaange. weka moto uwe kiasi ili dagaa wetu wasibabuke, wakishaiva na kubadilika rangi watoe uwaeke kwenye chombo wajichuje maji kwanza. dagaa wetu tayari