Jinsi ya kupika Sambusa za nyama


Ndugu wapenzi, Leo tunakuja na Jinsi ya kupika Sambusa Za nyama. Sambusa  Hupendwa na wengihasa za nyama. Sambusa ni Tamu sana, wengi hupenda kula pamoja na Juisi, soda na hata chai.

Mapishi ya Sambusa Za Nyama /Jinsi ya kupika sambusa hatua kwa hatua

Mahitaji

  • ½ kilo Nyama ya iliyosagwa
  • kijiko 1 kikubwa cha chakula cha Pilipili manga
  • Kijiko kimoja cha chakula cha kitunguu Thomu na tangawizi iliyosagwa
  • Mafuta ya kupikia Kiasi
  • Vijiko vinne unga ngano au ute wa yai kwa kufungia sambusa
  • Kaki za sambusa/manda/ chapati nyepesi (unaweza kununua zilizokuwa tayari zimeshakatwa kwa ajili ya sambusa au kama utanunua zile sheet pana utazikata kwa inchi 4 upana wa ruler yaani upate mistari 3

Directions

  1. Kausha nyama ya kusaga kwa kiyunguu swaumu (thomu) na tangawizi pamoja na chumvi mpaka ikauke vizuri Iwache ipoe.
  2. Kata kata majani ya kotmiri weka upande Kata kata upate vipande vidogo vidogo(chop) vya vitunguu maji.
  3. Zikate pili pili zako slice za mviringo vidogo vidogo.
  4. Wakati ukimaliza matayarisho haya na nyama yako itakuwa ishapoa kabisa hapo ndio utachanganya,bizari nzima pamoja na pilipili manga pamoja na vitu vyote ulivyokwisha vitayarisha
  5. Koroga unga ndani ya kibakuli au ute wa yai
  6. Weka kaki kwa mfungo wa triangle yaani pembe tatu kama kofia na
  7. weka mchanganyiko wa nyama yako kiasi na uanze kuzifunga sambusa zako na ukifika mwisho hapo ndipo upake unga wako kwa ajili ya kuifunga isifunguke wakati wa kuchoma, pendelea kutumia kaki 2 kwa kila sambusa moja.
  8. Kuchoma kwake ikiwa unazifanya na kuzichovya hapo hapo mafuta lazima yawe baridi (ninakusudia uweke mafuta na uzitie sambusa kabla hayajapata moto).
  9. Na ikiwa uliziweka kwenye friji zikaganda basi unatakiwa uzichome kwa mafuta ya moto
Muhimu
Watu wengi hupata usumbufu katika kufunga sambusa, Jaribu mara kwa mara utafanikiwa tu, ni kiasi cha kuzowesha mikono kufuatisha ile Triangle tu.
Pia waweza kutupia njegere kiasi zilizopikwa katika mchanganyiko wako wa nyama ili kupendezesha zaidi. Kama nilivyofanya katika sambusa zangu hapo juu.
Hivyo ndivyo Jinsi ya kupika Sambusa za nyama. Ahsanteni