Jinsi ya kutengeneza Kalimati ya maharage: Maharage yanatumika katika mapishi aina nyingi sana, Leo tutapika kalimati kwa kutumia maharage!. Kaimati hii ni nzuri sana kwani ina maharage yenye protini nyingi.
Pishi: jinsi ya kutengeneza Kalimati ya maharage
Maandalizi na Mahitaji
Ingredients
- Maharage yaliyopikwa na kuiva 1/2 kikombe.
- Maziwa safi 1/4 kikombe.
- unga wa ngano Kikombe kimoja.
- Mafuta ya kupikia.
- Chumvi kiasi.
- Yai 1.
- Baking powder 1/2 kijiko cha chai (ukipenda).
Utayarishaji
Jinsi ya kutengeneza Kalimati hatua kwa hatua
- Chemsha maharage hadi yalainike na kukauka maji.
- Maharage yakipoa songa hadi yalainike vizuri.
- Chukua Una wa ngano changanya na backing powder kisha chekecha na tia chumvi.
- Changanya unga na maharage katika bakuli kubwa safi
- Koroga yai.
- Tia yai katika mchanganyiko huo, changanya vizuri
- Tia maziwa kwenye mchanganyiko huo, hakikisha unakuwa mzito wa kutosha unaokatika ukimimina.
- Chemsha mafuta katika kikaangio chako.
- Chota na kijiko cha chakula weka kwenye mafuta yanayochemka.
- Choma mpaka ziwe za kahawia. Tayari kitafunwa.
- Unaweza kutumia sukari badala ya chumvi na kalimati zako zitakuwa tamu