Habarini wadau wa mapishi, leo nimewaandalia jinsi ya kupika vitumbua. Hiki ni kitafunwa kinachopendelewa sana kwa chai. unga utokanao na mchele ndio unaotumika.
Pishi: Vitumbua
Mahitaji
- mchele kilo 1
- nazi kubwa 2
- hiliki kiasi
- sukari robo kilo
- hamira kiasi kijiko kimoja nusu ( itategemea aina ya hamira)
- mafuta nusu lita
- mayai 3 (ukipenda)
Pishi la Vitumbua Hatua kwa Hatua
- uroweke mchele uliokwisha uchambua vizuri na kuupeta.
- utandaze sehemu safi ukauke, kisha usage upate unga mlaini
- kuna nazi uchuje tui zito
- saga hiliki, changanya na sukari
- changanya ule unga wa mchele, sukari, hiliki, tui la nazi na hamira. uvuruge uwe mwepesi kiasi cha kuweza kuchoteka kwa upawa. Acha uumue kwa dakika 25 hadi 30 kutegeme na ubora wa hamira.
- weka kikaango cha kukaangia vitumbua jikoni, anza kukaanga vitumbua vyako kwa kueka mafuta kwanza yapate moto, kisha unachota kwa upawa unga na kueka kwenye vijungu vya kikaangio chetu. unaacha vichemke upande mmoja, kisha unageuza upande wa pili, vikishaiva vitoe weka kwenye chujio ili mafuta yajichuje. Endelea kukaanga viliobakia mpaka unga uishe
Jinsi ya kupika Vitumbua. Kama una maoni yatupie hapo chini Asante