Jinsi ya kupika kababu za mayai


Habari wadau wa mapishi. Leo pishi letu ni la kababu za mayai, ni chakula kitamu sana ambacho chaweza kuliwa muda wowote, iwe mchana,asubuhi au hata jioni. chapendeza kusindikizwa na vinywaji baridi, ukijaaliwa kinywaji cha moto sawa na hata ukiwa na glasi ya maji kinaenda bila shaka.

Mahitaji

  • Mayai   7
  • Chenga za mkate
  • Nyama ya kusaga   robo kilo
  • Tangawizi nusu kijiko
  • Kitunguu thowm nusu kijiko
  • Mafuta ya kupikia nusu lita
  • Mkate
  • Chumvi kiasi
  • Pilipili manga kiasi

Jinsi ya kupika kababu za Mayai Hatua kwa Hatua

  1. osha mayai manne na kuyachemsha hadi yaive vizuri.
  2. changanya nyama, chumvi , tangawizi, thoum na pilipilimanga. chemsha hadi ikauke.
  3. loweka mkate ndani ya maji hadi uwe laini.
  4. Kamua mkate changanya na nyama.
  5. vunja mayai mawili, changanya vyema na nyama.
  6. menya mayai yetu tulochemsha. yanyunyizie unga wa ngano mayai ili yakauke.
  7. kila yai lilochemshwa lizungushie nyama sehemu zoote vizuri
  8. piga yai, chukua madonge yetu yenye nyama  ndani na uyachovye kwenye yai na kisha viringisha kwenye chenga za mkate, Kisha tia kwenye mafuta yanayochemka jikoni, zikishaiva na kubadilika rangi kuwa ya hudhurungi zitoe weka kwenye chujio zijichuje mafuta kwanza.
  9. Ziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
Haya wapenzi wa mapishi, kababu zetu hizo, kinywaji chaguo lako. mi nimeandaa na juisi, karibuni.

1 comments:

Naomba unitumie kwa email yangu hayo madikodiko