Jinsi ya Kupika Katlesi za Samaki



Habarini za muda huu wapenzi wa jinsi ya kupika. Jiweke tayari tuandae pishi letu la leo, katlesi za samaki. Ni miongoni mwa chakula kipendwacho na wengi kutokana na ladha yake. Haya sasa natumai upo tayari tuandae pamoja.

Mahitaji

  • samaki vipande viwili
  • viazi mbatata(mviringo) nusu kilo
  • mafuta lita 1
  • ndimu 2
  • vitunguu thoum
  • tangawizi
  • mayai 2
  • pilipilimanga ya unga
  • mdalasini wa unga kiasi
  • chumvi kiasi
  • uzile (bizari nyembamba) wa unga

Namna ya kuandaa na kupika Katlesi za samaki

  1. Osha viazi, vichemshe mpaka viive, kisha viache vipoe
  2. Menya viazi na uviponde viwe laini
  3. Msafishe samaki, mtie chumvi, thoum, tangawizi, pilipilimanga, mbandike jikoni akauke vizuri
  4. mchambuechambue samaki wako
  5. changanya samaki na viazi, chumvi, uzile, mdalasini, pilipilimanga, thoum, tangawizi, kamulia na ndimu.changanya vizuri
  6. Fanya vidonge vidonge vyenye umbo zuri
  7. piga mayai kwenye bakuli
  8. chovya katlesi kwenye mayai na kaanga kwenye mafuta ya moto. Tumia karai kukaangia
  9. ukipenda garagiza kwenye unga wa tosi kabla hujazikaanga
  10. zikishaiva, zitoe uzichuje mafuta, kisha uzitie kwenye sahani tayari
Naam, katlesi zetu za samaki tumeziandaa namna hiyo, karibuni