Jinsi ya kuandaa Kachumbari mchanganyiko

Jinsi ya kuandaa Kachumbari mchanganyiko


jinsi ya kuandaa Kachumbari mchanganyiko: Habari mpenzi wa blogu yetu, Leo tunakuletea namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko. Fuatana nami

Namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko hatua kwa hatua

Mahitaji muhimu

  • Nyanya kubwa 2
  • Vitunguu maji 3
  • Karoti 3
  • Pili pili hoho ya kijani 1
  • pilipili hoho nyekundu 1
  • Tango 1
  • Kotmiri 1/2 fungu(1/2 kicha ) au 1/2 bunch
  • Majani ya Iliki (parsley)  1/2 fungu (1/2 kichana) au 1/2 bunch
  • Cerely vijiti 4
  • Chumvi kiasi
  • Ndimu kiasi

Jinsi ya kuandaa/kutayarisha

  1. Osha mbogamboga kwa kutumia maji safi ya uvugu vugu (pendelea kuosha saladi kwa kutumia maji ya namna hii ili kuua vijidudu)
  2. Katakata vitu vyote isipokuwa ndimu, kisha uweke katika mashine ya kusagia chakula (yaani food processor)
  3. Weka namba mbili kwenye mashine yako kisha Saga mchanganyiko wako kwa kusita sita kila baada ya sekunde 1 mpaka kachumbari yako ichanganyike vizuri.
  4. Ikishachanganyika vizuri, Weka maji ya ndimu kisha changanya na kijiko, Tia ndani ya bakuli tayari kwa kuliwa
Vilevile waweza kutumia brenda kwa ajili ya kusagia, hakikisha usisage kwa muda mrefu ili isiwe majimaji sana. Hivyo ndio namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko. Asanteni!