Za muda ndugu zangu, leo tuandae kitu cha kuchapuzia bajia. Hii ni chatne ya nazi, maarufu na inakupa hamu ya kula bajia zako, ziwe za dengu au zile bajia za kunde ( vikababu)
Mahitaji
- nazi 1
- pilipili mbichi 3
- ndimu kiasi
- chumvi kiasi
Kuandaa chatne Hatua kwa Hatua
- kuna nazi halafu uisage iwe laini sana
- saga pilipili na chumvi kisha changanya vyote pamoja kwenye nazi
- kamulia ndimu yako, chatne tayari