Katless za nyama kati


Katless ni miongoni mwa vitafunwa vyenye kuvutia, waweza zipika kwa nyama ya kusaga au hata samaki hupendeza na zina ladha nzuri. Leo katless zetu ni za nyama ndani, haya twende hatua kwa hatua.

Ingredients

  • Viazi nusu kilo
  • nyama ya kusaga robo kilo
  • thoum na tangawizi kiasi
  • pilipili manga kiasi
  • bizari nyembamba kidogo
  • vitunguu maji 2
  • ndimu 1
  • karoti 1
  • mayai 2
  • chumvi kiasi
  • mayai 2
  • mafuta lita1

Directions

  1. Chemsha viazi , vikishaiva viepue uvimenye, kisha uviponde
  2. Safisha nyama kisha uitie viungo, thoum, tangawizi, pilipili manga na chumvi. Ibandike jikoni iive na ikauke vizuri.
  3. Saga karoti, kata vitunguu vidogodogo utie kwenye viazi uloviponda. Tia bizari nyembamba, chumvi na ndimu, thoum na tangawizi kiasi navyo changanya kwenye viazi vyetu. Na kama unatumia pilipili tia ilosagwa itanoga
  4. Tengeneza vidonge vya viazi, weka vishimo kati utie nyama tuloikausha, kisha ifunike vizuri kwa viazi.
  5. Bandika mafuta jikoni yakishapata moto chovya katless zetu kwenye yai  lilopigwa kisha zitie kwenye mafuta ukaange. Ukipenda, ukishazichovya kwenye yai zigaragize kwenye unga wa tosi kisha ndo uzikaange kwenye mafuta. Kumbuka kutumia karai kukaangia ili katless ziweze kudumbukia kwenye mafuta vizuri.
  6. zikishakaangika na kubadilika rangi kuwa hudhurungi ya mbali, zitoe uzitie kwenye chujio zijichuje mafuta, kisha zitie kwenye sahani, tayari kwa kuliwa
Katless zetu tayari, kama kuna juisi pembeni heri. La ikikosekana hata maji unashushia sio mbaya. Kitafunwa hiki kinalika asubuhi, jioni na hata mchana. Karibuni