Jinsi ya kupika Donats: Karibuni tena wadau wa jinsi ya kupika. Leo tuandae donats, hiki ni kitafunwa kipendwacho na wengi. Donats zinapendeza zikisindikizwa na chai, maziwa, kahawa, juisi na hata maji. Haya sogea karibu uweze kufatilia hatua kwa hatua.
Mahitaji
- Unga wa ngano kilo 1
- siagi robo kilo
- mafuta ya kupikia lita 1
- sukari ilosagwa robo kilo
- maziwa robo lita
- kungumanga kijiko 1 cha chai (ukikosa tumia mdalasini ulosagwa )
- mayai 3
- baking powder kijiko 1 kikubwa
Jinsi ya kutengeneza Donats hatua kwa hatua
- Changanya unga na baking powder pamoja na siagi hadi unga uchanganyike
- tia sukari kidogo, kungumanga na yai kisha endelea kuchanganya unga. Weka maziwa na kanda mpaka upate donge laini
- tengeneza madonge, uanze kusukuma unga kiasi cha sentimeta moja. Usiwe mwembamba sana kama wa chapati.
- kata duara kwa glasi au kikombe kisha kata duara lingine dogo katikati kwa kutumia kifuniko cha chupa ya maji au kitu chochote chenye duara dogo, upate shepu ya ringi.
- Bandika mafuta jikoni, yakipata moto tia donats uzikaange mpaka ziwe na rangi nzuri, zikishaiva epua, zichuje mafuta kisha garagiza kwenye sukari ilosagwa kabla hazijapoa
- zitoe uziweke kwenye sahani tayari kumfikia mlaji