Jinsi ya kutengeneza biskuti za Ufuta


Jinsi ya kutengeneza biskuti (biscuit) za ufuta: Nimechagua kupika biskuti hizi kwa sababu kuu mbili. Kwanza ni rahisi sana kutengeneza na hazihitaji viungo vingi (mahitaji yake ni machache), Pili ni tamu sana. Nafikiri na wewe utazipenda.

Pishi: Biskuti za ufuta

Maandalizi na Mahitaji

Mahitaji

  • Unga wa ngano gramu 450 (kama vikombe 3 vya vya chai)
  • Sukari ya kusaga 1/4 Kikombe
  • Siagi 250 gramu (kama kikombe 1 na nusu)
  • Mayai 3
  • Jam kiasi
  • Ufuta gramu 120 (kama 3/4 ya kikombe)
  • Vanilla 1 kijiko cha chai

jinsi ya kupika

  • Changanya Siagi na sukari kwa kutumia Blenda au machine ya kutengenezea keki. Hakikisha imechanganyika vizuri.
  • Ongeza yai moja huku ukiendelea kuchanganya, kisha ongeza vanilla.
  • Tia mchanganyiko wako katika bakuli safi, Tia baking powder, na unga na changanya kwa mkono vizuri.
  • Paka siagi chombo (sinia) ya kupikia ya oveni.
  • Tengeneza viduara vidogo vidogo.
  • Bonyeza katikati ya kila kiduara kwa kidole, kisha weka jam, halafu juu yake paka mayai na unyunyuzie ufuta.
  • Pika katika moto wa chini 350ºF kwa muda wa dakika 20-25.
  • Tayari kwa kuliwa.

Biskuti za ufuta: Dondoo
Waweza kutengeneza miundo mbalimbali kama pembe tatu, kopa nk kulingana na ubunifu wako
Hivi ndivyo kwa ufupi namna ya kutengeneza Biskuti za ufuta ningependa kusikia kutoka kwako, weka maoini yako hao chini