Jinsi ya kupika keki ndogo za rangi


Jinsi ya kupika keki ndogo za Rangi na Icing: Zulfa ni Mwanafunzi wa Chuo fulani Jijini Dar es salaam na ni mpenzi mkubwa wa blogu hii.
Leo anatuletea pishi la keki fuatana nae…
Katika vyakula ambavyo napenda nipate walau mara moja kwa mwezi ni Keki. Nilipokuwa mdogo bibi yangu ambaye alikua akifanya kazi za ndani kwa wahindi alinifundisha mapishi mbalimbali. Moja ya mapishi hayo ni keki hii ninayoiandika sasa, Nimeviita vikeki kwa sabau ni vidogo vidogo na vinatoka vingi katika mpiko mmoja.

Jinsi ya kupika keki ndogo za icing; Hatua kwa hatua

Mahitaji

  • Unga wa ngano                              Kikombe kimoja na nusu
  • Maziwa                                             Robo Tatu ya Kikombe
  • Siagi isiyo na chumvi               Nusu Kikombe
  • Hamira (Bakin powder)         Kijiko kimoja cha chai
  • Chumvi                                          Nusu Kijiko cha chai
  • Sukari                                              Kikombe Kimoja
  • Mayai                                               3
  • Vanilla                                              Kijiko Kimoja na nusu cha chai

Namna ya Kutengeneza keki hatua kwa hatua

  1. Kwanza washa tanuri (oveni) kwa kiasi cha nyuzi joto 350°. Kisha weka karatasi za kupikia keki za vikombe kwenye trei.
  2. Tia Unga, Baking powder na chumvi katika Bakuri safi, halafu Changanya pamoja na uuweke kando mchanganyiko wako huo.
  3. Tia siagi na sukari katika bakuli la mashine changanya hadi ilainike vizuri.
  4. Wakati mchanganyiko wa siagi na sukari ukiendelyea kulainika, tia yai moja baada ya jingine huku unaendelea kuchanganya, halafu tia vanilla.
  5. Huku unaendelea kuchanganya, tia nusu ya mchanganyiko wa unga uliyoweka kando (katika hatua ya pili juu),
  6. kisha tia maziwa na umalizie na mchanganyiko wa unga uliyobakia.
  7. Ikisha changanyika vizuri, mimina kwenye karatasi za kuchomea keki za vikombe. Hakikisha usijaze mpaka juu.
  8. Weka katika oveni acha iive kwa muda wa kama dakika ishirini.
  9. Ziache zipoe. Zikisha poa zipake icing/cream upendayo na keki zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Mapishi ya keki hii: Dondoo
Utayarishaji huu unaweza kutoa keki ndogo 12. Waweza kuongeza au kupunguza kulingana na mahitaji yako
Hivyo ndivyo jinsi kupika Keki(vikeki) ndogo za Icing. usisite kutoa maoni hapo chini. Asante!