Jinsi ya kupika mchuzi wa kababu

jinsi ya kupika mchuzi wa kababu


Habari zenu wanajiko letu, leo tuandae mchuzi wa kababu za nyama ya kusaga. Mchuzi huu ni mzuri sana usikose hatua kwa hatua.

Mahitaji

  • Nyama ya kusaga nusu
  • viazi mbatata robo
  • vitunguu robo
  • mafuta ya kula nusu kikombe
  • nyanya 5
  • tangawizi kiasi
  • thoum kiasi
  • Uzile kidogo
  • mdalasini na hiliki kiasi
  • majani ya kotmiri kiasi
  • limau 1
  • chumvi kiasi

Jinsi ya kuandaa mchuzi hatua kwa hatua

  1. Safisha nyama, iweke katika chujio ivuje maji
  2. andaa vitunguu, nyanya, saga thoum, tangawizi na mdalasini, hiliki na uzile visage pia. Kotmiri zioshe uzichambue.
  3. tia nusu ya viungo ulivyosaga na tangawizi na thoum kwenye nyama, weka na limau kisha ufinyange vidonge kama kababu.
  4. bandika sufuria  jikoni tia maji kiasi, yakishashemka vizuri, tia zile kababu tuliotengeneza, wacha zichemke hadi zishikane kisha ziepue uchuje maji. Lakini maji ulochuja usiyamwage
  5. bandika sufuria jikoni, tia mafuta, yakipata moto weka vitunguu ukaange, vikibadilika rangi tia nyanya na thoum na viungo vyote vilobakia. Tia na kotmiri endelea kukaanga.
  6. kata viazi vyembamba uvitie uendelee kukaanga mchuzi wetu. Tia kababu, chumvi na limau, wacha vichemke viazi viive, na yale maji tulochuja kidogo yatie. Viazi vikiiva na mchuzi ukawa sawa epua tayari
Unaweza kutumia mchuzi wa kababu pamoja na tambi, wali na hata mikate. Natumai tumelifurahia pishi letu la mchuzi wa kababu. Kwa maoni na ushauri mnakaribishwa sana