Habari, leo jikoni tuna kisamvu, kisamvu chetu kitaungwa kwa nazi. Ni mboga nzuri inayoenda vyema kwa wali, ugali na hata mikate. Karibuni tuandae mboga yetu.
Pishi: Kisamvu cha Nazi
Mahitaji
- Kisamvu fungu kubwa 1
- nazi 2
- vitunguu maji 2
- vitunguu thoum kiasi
- mafuta kidogo
- chumvi kiasi
Jinsi ya Kuandaa na Kupika Kisamvu cha Nazi hatua kwa hatua
- Kichambue kisamvu, ukikoshe, kisha ukitwange kilainike. Inapendeza ukikitwanga ukiwekee vitunguu thoum na pilipili kama unatumia.
- kichemshe mpaka kiive, kikauke
- bandika sufuria, weka mafuta yakipata moto weka vitunguu kaanga, kisha weka vitunguu thoum, tia mboga yetu
- Weka chumvi na tui zitozito, wacha ichemke hadi tui likauke, mboga tayari