Jinsi ya kukaanga samaki wa masala

jinsi ya kukaanga samaki wa masala
  • Unataka kujua Namna ya Kukaanga Samaki?:Samaki ni miongoni mwa vyakula vyenye protin, ambayo ni muhim katika kujenga mwili. Naam, samaki aweza pikwa kwa ufundi tofautitofauti ili mlaji uweze kufurahia chakula chako, kaanga, mchemshe, mbanike yote mapishi ya samaki. Leo tuanze na samaki wa kukaanga, sote twaijua ladha yake, kwa ugali, wali, viazi, mikate na hata wenyewe tu na pilipili yako pembeni.

Mahitaji

  • Samaki vipande 6
  • mafuta nusu lita
  • mayai 2
  • ngano nusu kikombe
  • chenga za mkate kiasi
  • pilipili manga kiasi
  • chumvi
  • vitunguu thoum
  • Tangawizi kiasi
  • limau kubwa 1
  • pilipili mbichi (kama unapenda)

Jinsi ya Kukaanga samaki Hatua kwa Hatua

  1. Safisha vipande vya manofu ya samaki, ondoa miba.
  2. saga vitunguu thoum na tangawizi, katakata pilipili  vipande vidogodogo.
  3. kamua limau, changanya na viungo vyote ulivyosaga kisha tia kwenye samaki. Tia na chumvi kiasi kisha uache Viungo vichanganyike na samaki kwa kiasi cha dakika ishirini (20).
  4. Andaa mayai kwa kuyapiga na kuyaweka katika chombo kisafi.
  5. viviringishe vipande vya samaki kwenye ngano, kisha vichovye kwenye mayai, baada ya hapo viviringishe kwenye chenga za mkate
  6. Vidumbukize kwenye mafuta yanayochemka, kaanga samaki hadi waive na kubadilika rangi kuwa hudhurungi. Hapo watakua tayari waeke pembeni
Naam, natumai ukiweka na chips au viazi pembeni vinaenda. Karibuni sana kwa maoni na mapendekezo hapo chini