Jinsi ya kupika uji wa viazi vitamu: Shukurani nyingi kwa Mama Salmin mpenzi wa blogu hii kwa kututumia pishi hili. Je unajua kuwa waweza pika uji mtamu kwa kutumia viazi? fuatilia…
Pishi: Uji wa Viazi vitamu
Maandalizi
Mahitaji
- Unga wa viazi vitamu kijiko cha chakula 1.
- Unga wa soya kijiko cha chakula 1.
- Unga wa mahindi vijiko vya chakula 4.
- Limau 1
- Sukari vijiko vya chai 2.
- Maji vikombe 6
Utayarishaji na upishi
jinsi ya kutengeneza uji hatua kwa hatua
- Weka chombo safi cha kupikia jikoni, tia vikombe vitano vya maji acha yachemke.
- Changanya unga wa soya na unga wa mahindi kwa kutumia kikombe kimoja cha maji kilichobaki ili kufanya uji mzito.
- Weka mchanganyiko wako huo kwenye maji yanayochemka huku ukikoroga kuzuia unga kushikana na kuwa mabonge. Kisha acha uchemke kwa dakika kama 20.
- Wakati sufuria ikichemka, tengeneza juisi ya limau
- Baada ya dakika 20 Uji uliopikwa utakuwa mzito, ondoa uji kwenye moto na ongeza juisi ya limau na sukari.
- Poza, tayari kwa matumizi.
My rating
Jinsi ya kupika uji wa viazi vitamu: Vidokezo
- Maziwa yanaweza kuongezwa ikibidi,
- Waweza kutumia unga wa ulezi, mtama au Muhogo badala ya unga wa mahindi.
- Muda halisi wa kuiva uji huu inategemea na ukali wa moto na aina ya unga unaotumia.
1 comments:
Nashukuru kwa somo, vip faida zake mwilini ni zipi? Napenda kujifunza zaid