Jinsi ya kuandaa mishikaki ya kuku


Jinsi ya kuandaa Mishikaki ya kuku: Habari za leo wapenzi wa blogu yetu hii. Leo napenda tuandae pamoja pishi hili. Kwa mara ya kwanza Mishikaki ya kuku niliionja nikiwa safarini visiwani Zanzibar, baada ya kurudi nyumbani nikawa najaribu kuandaa kwa namna tofauti tofauti. Leo nimeamua kutafuta namna nyepesi ya kuandaa mishikaki hii ya kuku. Fuatana nami.

Pishi: Mishikaki ya kuku

Maandalizi

Mahitaji

  • Kuku mchanga 1 (broiler)
  • Bizari nyembamba kijiko kikubwa cha chakula kimoja
  • Kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja na nusu
  • Pilipili manga kijiko kimoja cha chai (iliyosagwa)
  • Pilipili mbuzi iliyosagwa Robo kijiko cha chai
  • Ndimu kubwa Moja (kamua)
  • Bizari ya manjano Robo kijiko cha chai
  • Curry powder nusu kijiko cha chakula
  • Chumvi kiasi

Utayarishaji na upishi

Jinsi ya kuandaa mishikaki ya kuku hatua kwa hatua

  1. Kata kuku wako vipande vidogo vidogo kiasi kisha vioshe vizuri.
  2. Changanya vipande vya kuku pamoja na viungo vyote.
  3. Koroga vizuri mpaka uhakikishe vipande vya kuku vimechanganyika vizuri na viungo vyote kisha acha kwa dakika tano.
  4. Tunga vipande vya kuku kwenye vijiti vya kuchomea mishikaki.
  5. Choma mishikaki mpaka iwive vizuri hakikisha isikauke ikawa mikavu sana.
  6. Itoe na uweke kwenye sahani Mishikaki ya kuku itakua tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kuandaa Mishikaki ya kuku: Vidokezo

  • Ukimuacha kuku akauke sana atatoka ladha
  • Waweza kutia nusu kijiko cha pilipili iliyosagwa kama utapenda
  • Mishikaki hii itapendeza sana kama italiwa na sauce ya ukwaju na saladi.
Hivyo ndio namna ya kuandaa mishikaki ya kuku asanteni.