Jinsi ya kupika Bamia na Karanga: Umewahi kula ugali kwa
bamia? unajua namna ya kuandaa bamia tamu na karanga? Leo nimewaandalia
pishi hili la kiswahili la kiasili, Tuwe pamoja
Pishi: Bamia na karanga
Maandalizi na Mahitaji
Mahitaji
- Bamia mbichi
- Kitunguu maji
- Karanga zilizo kaangwa
- Nyanya
- Binzari
- Vitunguu swaumu
- Chumvi kidogo
- Maji ya kutosha
- Limau au ndimu
jinsi ya kupika
jinsi ya kupika bamia na karanga hatua kwa hatua
- Andaa karanga kwa kuzikaanga na kisha kuzitwanga au kusaga ili kupata unga
- Safisha na pauza/kwangua bamia, kata sehemu kidogo za mwisho na zitupe shambani ziwe mbolea. Zikatekate bamia vipane vidogo vidogo
- Menya nyanya kuondoa maganda kama ni lazima au sivyo osha nyanya katakata vpande vidogo vidogo pamoja na maganda yake
- Weka bamia, vitunguu, nyanya, binzari na chumvi kwenye chungu au sufuria. weka maji yanayocheaka ya kiasi tu.
- Bandika jikoni, endelea kupika mpaka mchanganyiko uive kidogo (dakika 10). Ongeza matone machachae ya limao au ndimu.
- Changanya maji kidogo ya moto na karanga, ongeza kwenye chugu au sufuria yenye bamia.
- Endelea kupika kwa moto mdogo kwa dakika tano huku ukiendelea kukoroga kila mara. Ongeza maji ya moto kama yanahitajika.
- Hakikisha mboga na karanga vimeiva na karanga hazikuungulia kwenye kitako cha sufuria au chungu
- Epua na andaa tayari kwa kuliwa
- Kwa kuongeza mvuto wa mboge yako waweza tupia pilipili nyekundu, korosho kama 8
- Kuongezea ladha waweza kuweka maziwa ya mgando(mtindi) wakati unapika.
- Waweza kula mboga ya bamia pamoja na Ugali wa mahindi, muhogo au mtama.